WELCOME NOTE

WELCOME NOTE

PICHA

PICHA

TANGAZO

Wednesday, September 5, 2012

DHANA NA MAANA YA ISTILAHI MBALIMBALI ZINAZOTUMIKA KATIKA SOMO LA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA


      a)      KUFARAGUA
Ni ubunifu wa kutengeneza zana kwa kutumia vifaa au makunzi yasiyohalisi na yanayopatikana katika mazingira husika.Ufaraguzi unaweza ukawa wa namna hizi;
  •       Kutumia kitu papo kwa papo kinyume na matumizi yake ya kawaida.Mfano,unapotumia penseli kama kishikizi katika kupigia mstari(hapa utakuwa umeitumia penseli kama rula.Ama vile,
  •   Kutumia malighafi/vifaa au makunzi zinazopatikana katika mazingira yetu husika(ama kwa kuokota au kuzitafuta) katika kutengeneza vifani mbalimbali(zana ) kwa gharama nafuu. Zana nyingi zinazobuniwa,faraguliwa na kutengenezwa  hutumia vifaa vinavyopatikana katika mazingira yetu husika.Mfano unaweza;
(a)    Kutengeneza vifani vya viumbe hai kwa kutumia udongo(kufinyanga)
(b)   Kutengeneza mpira kwa kutumia vitambaa /makaratasi ya nailoni.(kushona)
(c)    Kutengeneza kisu kwa kutumia miti(kuchonga) nk.

      b)      MAKUNZI
Malighafi zinazotumika katika kutengenezea kitu au zana.Vifaa hivi vinaweza vikawa vya kuokota ama kununua.Mfano unaweza ukaokota mimea,maboksi,makopo nk.Pia unaweza ukanunua kadi za manila nk.


     c)       ZANA MPITISHO
Ni zana zinazotumika katika kupitishia maarifa yanayotolewa darasani katika swala  zima la ufundishaji na ujifunzaji.Mfano ubao wa chaki,Luninga nk.Ieleweke kama si ubao ama chaki ndivyo vinavyopitisha maarifa,bali ni “Ubao wa chaki”,kwani unaposema “Ubao “ni neno pana sana na linaweza likatumika katika miktadha mbalimbali,kinyume na unaposema ubao wa chaki, hapa moja kwa moja utakuwa umeiweka dhana hiyo katika muktadha wa ufundishaji na ujifunzaji.Pia chaki, haipitishi maarifa yoyote zaidi ya kutumika katika kuandikia katika ubao.

      d)      KIVUNGE CHA SOMO
Kisanduku cha mbao /bati kilichotengenezwa kwa  ajili ya kuhifadhia zana.Ifahamike  kuwa ,zipo baadhi ya zana ambazo ni rahisi kuharibika,na zingine ni hatari kwa binadamu (kama viviminika vya kemikali),na baadhi ni gharama.Kwa muktadha huu,mwalimu huna budi kuhifadhi zana zako katika mazingira yatakayokupelekea kuvitumia tena baadaye na kutoleta madhara yoyote kwa watumiaji .
 
      e)      TEKNOLOJIA
Maarifa ya sayansi yaliyowekwa kwenye matumizi ya vitu kama vile zana.Tunaamini kuwa kwa Dunia ya sasa,kila eneo linaihusisha teknolojia katika uendeshaji wake.Kwa mfano katika maswala ya biashara,kiuchumi nk. Sekta ya Elimu pia, hutumia teknolojia katika uendeshaji wa shughuli zake. Matumizi ya teknolojia katika zana nayo yanachangia ubora wa elimu yetu na kurahisisha swala zima la ufundishaji na ujifunzaji.Tunaweza kuona namna ya zana mbalimbali za kisasa kwa mfano luninga,kompyuta, projekta, intarneti, na mfumo wa mawasiliano ya kimkutano(teleconference system) zinatumika katika kurahisisha tendo zima la ufundishaji na ujifunzaji.Matumizi haya ya teknolojia yanahitaji ujuzi wa hali ya juu ili kuleta ufanisi katika suala zima la ufundishaji na ujifunzaji.

      f)       KIFANI
Kitu kinachofanana au kushabihana na kingine.Kuna aina kuu mbili za vifani;
a.       Vifani vya viumbe hai(zana zilizotengenezwa kwa kuzingatia mifano ya maumbo mbalimbali ya viumbe hai).Mfano,unaweza ukatengeneza mfano wa  mtu kwa kutumia udongo na si kumtengeneza mtu halisi(hivyo hushabiana na uhalisia wa kitu kilichotengenezwa) ama kuchora picha ya mfano wa simba,twiga nk.Vivyo hivyo nazo zitawakilisha mfano au kushabiana na maumbo ya wanyama hao.
b.      Maumbo yenye ukumbi kama vile mche duara,mche mstatili,tufe na vingine vingi.Hapa ni zile zana zilizotengenezwa kushabiana ama kufana na maumbo mbalimbali yenye ukumbi kama mche mduara.Mfano,unaweza kutengeneza umbo la mstatili kwa kutumia boksi.Umbo hili litafanana/kushabiana na umbo halisi la mstatili.

15 comments:

  1. Naomba nisaidiwe aina nne za ubao wa kufundishia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Zipo aina mbalimbali kama
      .ubao wa chaki-ule unaotumika zaidi madarasani ukiwa umepachikwa ukutani
      .ubao wa fulana - Mara nyingi hutengenezwa kwa kutumia kipande cha blanketi. Watoto huweza kubainisha herufi au namba na zilizobandikwa chanacnana Dume na kuzipachika katika aina hizo za mbao.
      .magnetic board - Ni zile mbao zenye mnato ambazo mwanafunzi anaweza kutumia stencil zilizoandaliwa kwa muundo wa vitu mbalimbali na kuzibandika katika mbao hizo wakati wa ujifunzaji.

      Delete
  2. .Ubao wa chaki
    .Ubao wa fulana (flannel board)
    .magnetic board

    ReplyDelete
  3. Asanteni Sana!

    Sikujua ntajibiwa mapema..nmefurahi!

    ReplyDelete
  4. Naomba pia nisaidiwe hatua za kuchukua wakati unataka kutumia radio kama zana darasani

    ReplyDelete
  5. Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kutumia ubao wa chaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba nisaidiwe tofauti kati ya chati na mabango

      Delete
  6. Mambo ya kuzingatia wakati was kutumia ubao:
    -hakikisha kuwa ubao hauna maandishi mengine
    -gawa ubao kwa kuzingatia ukubwa wake, standard huwa ni sehemu tatu
    -wakati was kuandika usiwape mgongo wanafunzi simama upande
    -wakati was kuandika usiwe karibu sana wala mbali sana,sm 30 toka ukutani na mguu wako
    -unapoandika usilaze shingo au kichwa utapindisha mistari
    - andika ubaoni kwa kuzingatia kimo chako
    -tumia rula kwa kazi zote za ubao
    Chaki za ranging zitumike kuchorea michoro na kupiga mistari
    -Futa ubao baada ya kumaliza kazi ya ubao nk.
    Rejea,TET,(2000) mitaala na zana za
    kujifunzia,TET,Dar es salaam65-69.

    ReplyDelete
  7. Naomba kuuliza zana mafunzo Ni zipi na zana msingi Ni zipi?

    ReplyDelete
  8. Naomba kujua makundi ya vielelezo na teknolojia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yapo 3
      kundi la v/t maono
      Masikizi
      Masikizi-maono

      Delete
  9. Naomba kusaidiwa aina nne za ubao

    ReplyDelete
  10. Naomba kujua faida ya kutumia zana za kisasa katika kufundisha na kujifunzia

    ReplyDelete
  11. Naomba kusaidiwa kutambua sifa za makunzi boraa

    ReplyDelete
  12. Naomba kusaidiwa tofauti Kati ya vielelezo natekinolojia maono na makundi mengine




    ReplyDelete