WELCOME NOTE

WELCOME NOTE

PICHA

PICHA

TANGAZO

Tuesday, April 16, 2013

UTUNZAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA KWA KUFUNDISHIA NA KUJIFUNZIA


Dhana.
Ni hali ya kuweka vielelezo katika mazingira sahihi na yaliyo mazuri au salama ili kuhifadhi kutokana na uharibifu wa aina yoyote ule.

 Waharibifu wa vielelezo.
Waharifu wa vielelezo vya kufundishia/ kujifunzia ni wengi ikiwa ni pamoja na mikono ya watu wenyewe. Waharibifu wengine ni hali ya hewa, upepo, vumbi, wadudu waharibifu n. k.

Hali ya hewa
Ni moja kati ya waharibifu wa zana au vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Athari zinazosababishwa na hali ya hewa ni kubabuka rangi kwa chati au picha inapobandikwa kwa muda mrefu hupoteza nuru ya rangi.
Aidha hali ya hewa baridi husababisha ukungu kwenye vifaa ambavyo havikuhifadhiwa vizuri mfano kanda za video, kanda za kinasa sauti  n.  k. Hivyo basi mara baada ya kutumika mwalimu anatakiwa kuvihifadhi ili visiharibike.

Upepo na vumbi
Upepo unapeperusha chati na picha zilizopachikwa ukutani na juu ya ubao husababisha kuchanika. Upepo pia hupeperusha vumbi ambalo huaribu vitu kama vide, redio, kanda za sauti  n. k. Iwapo vifaa hivi havikuhifadhiwa vizuri vinaweza kuharibika.

Wadudu waharibifu
Mfano mchwa, mende, panya  n.k.Mwalimu analazimika awe muangalifu sana juu ya wadudu hawa kwani ni wadudu hatari sana kwa kuharibu zana za kufundishia.

 NJIA ZA UTUNZAJI WA VIELELEZO NA TEKNOLOJIA
Katika utunzaji wa vielelezo na teknolojia kwa kufundishia/ kujifunzia. Vielelezo vinaweza kugawanyika katika makundi mawili (2)
(i)                  Vinavyowekeka kwa muda mrefu
(ii)                Vinavyowekeka kwa muda mfupi

Vinavyowekeka kwa muda mfupi ni kama:- matunda, dagaa, aina mbalimbali za mboga za majani, hizi hutumika kwa muda mfupi na kutupwa jalalani na vile vinavyowekeka kwa muda mrefu, viwekwe kwa utaratibu mzuri ili visiharibike
 Njia zifuatazo zinaweza kutumika katika kuhifadhi vielelezo:-
(i)                  kuhifadhi katika visanduku au masanduku maalumu.
(ii)                Kuviweka katika kabati kutokana na wadudu waharibifu
(iii)               Kuviweka katika mifuko ya plastiki na kufungwa vizuri ili hewa isipite ambayo hatimaye huenda ikasababisha uharibifu
(iv)             Kutumia mikebe isiyopenyeza hewa. Hii inaweza kuhifadhi lenzi za projekta au projekta yenyewe na vitu vidogovidogo vinavyoharibika kwa ukungu vihifadhiwe katika mikebe hiyo au katika mikoba yao
(v)               Kuvisafisha na kuviangalia mara kwa mara
(vi)             Njia ya kugandishwa kwenye karatasi ngumu na kufanya fremu kwa mfano chati au picha zilizochorwa kwenye karatasi nyepesi zinaweza kubandikwa, kuninginizwa juu ya ukuta wa darasa
(vii)            Kuviweka katika chumba maalumu.
(viii)          Vipangwe vizuri ili visigongane au kujeruhiana.

No comments:

Post a Comment